MPYA ZA JACKIE CLIFF KUTOKA MAHABUSU MACAU CHINA!


Habari za Super Star Model Jacky Cliff aliyeko Rumande huko Macau/China kwa kunaswa na Sembe ni kwamba hatanyongwa ila atakula at least mvua 16, halafu majuzi ameambiwa rasmi kwamba kesi yake haitaanza mpaka baada ya Mwaka Mmoja na Nusu au Miwili inategemea itamchukua muda gani kujifunza Kireno lugha ya Taifa ya Macau.
               
 Sheria ya kisiwa hicho inasema kwamba hakuna mshitakiwa yoyote katika Taifa hilo aatakayepelekwa mahakamani mpaka Mahakama iridhie kwamba anajua Lugha hiyo ya Taifa inayotumika Mahakamani na si vinginevyo. Kwa hiyo Jacky ameambiwa kwamba aaanze sasa kujifunza lugha hiyo akiielewa kwa haraka ni bora kwake ila Sheria inatoa Mwaka Mmoja mpaka Miwili kujifunza lugha hiyo kwa ufasaaha. 

                  Jackie wakati wa harusi yake na Aliyekuwa Mume wake Abdullatif ambaye naye alitumikia kifungo cha miaka kadhaa Tanzania kwa kosa la kupatikana na sembe.

Habari zaisi za mtaani zinasema Super Model huyo amekuwa kijihusisha na shughuli hizi kwa takribani Miaka 5 sasa na kwamba amekuwa na tabia ya kuitumia kidogo kidogo sembe hiyo

 Jackie akiwa na anayesemekana kuwa ni Boyfriend wake mwanamuziki wa kizazi kipya JUX ambaye kwa sasa inasemekana anasoma China Pia.

Siku ya siku ilipotimia inasadikiwa alikuwa wamevuta kidogo kutokana na kosa kubwa alilolifanya la kuingia VIP ya Uwanja wa Ndege wa Macau huku akijua wazi kwamba hana Tiketi ya kwenda huko kwa wanene, kucha mengine ya kuchomewa mapema na maadui zake hilo peke yake iliwashitua sana Askari wa Usalama uwanjani hapo na kuanza kumtilia shaka sana na hasa panic aliyoionyesha baada ya kurudishwa kutoke VIP ndipo alipoishia kunaswa live amejilipua na sembe kibao tumboni mwake.